Quantcast
Channel: YALIYO JIRI MKOANI RUVUMA NA MKONGWE WA HABARI ADAM NINDI
Viewing all 441 articles
Browse latest View live

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA KATIKA MACHIMBO YA DAR PORI NA MPAKA WA MSUMBIJI

$
0
0
Wananchi wa Kijiji cha Nyoni kata ya Nyoni wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma wakiendelea a shughuli za ujasiliamali katika kujitafutia pato la kukidhi familia.
Waachi hao walifurahi kumuona Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhadisi Dkt Biilith Mahege akiwatembelea katka maeneo yao ya uzalishaji mali na kuwasisitiza kufanya shughuli za Maendeleo wakati alipokuwa ziara wilayai Nyasa hivi karibui.
Hapo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Mahenge akikagua shughuli za Ununuzi wa mahindi katika kituo cha kununulia Mahindi cha Tingi wilayani Nyasa, wananchi wameiomba Serikali iongeze kiwango cha ununuzi kutoka Gunia 500 hadi kufikia gunia 1000 kwa vijijini kwa kuwa uzalishaji ni mkubwa..
Akiwa Ziarani wilayani Nyasa Dr Mahenge alikagua shughuli mbalimbali za mendendeleo na namna wananchi wanavyohudumiwa na viongozi wanaosimamia utekelezaji wa maagizo ya serikali katika kuwatumikia.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Mahenge
Wananchi wa Wilaya ya Nyasa wakitumbuiza ngoma ya Kihoda wakati walipotembelewa na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuona changamoto zinazowakabili na hali ya chakula katika Msimu huu wa kilimo wa 2015/2016.
Dr Mahenge akisalimiana na wananchi na viongozi wa chama na Serikali waliojitokeza kumsikiliza alipotembelea wilayani Nyasa.
wananchi wakimkaribisha Mkuu wa mkoa kwa Ngoma na furaha

Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Mahenge ukiingia katika Eneo la Machimbo ya Dar Pori wilayani Nyasa
Wananchi wa Dar Pori wakifurahia kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvua
Mkutano wa Hadhara baina ya viongozi wa wilaya ya Nyasa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na wananchi wa Dar Pori.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge ametoa agizo kwa wakazi wa dar Pori kuheshimu sheria za mipakani na kutokuingiza Siasa  pakani.

Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini Nchini Msumbiji ameuomba Uongozi wa Serikali mkoa wa Ruvuma kuwaomba wachimbaji wanaotoka Tanzania kuacha kuingiza mambo ya Siasa katika Mipaka ya Tanzania na Msumbiji.

Mwenyekiti wa Wachimbaji kutoka Nchi Jirani ya Msumbiji  katika mpaka wa Dar – Pori na Turo Msumbiji ameyasema hayo wakati alipokaribishwa katika kumpokea Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge aliyetembelea katika Makazi ya Wachimbaji wa Dar pori Wilayani Nyasa.


Amemwomba Mkuu wa Mkoa kuendeleza amani hiyo kwa kukemea watu wanaogeuza  Mipaka kuwa sehemu ya Siasa. Mwenyekiti huyo alitoa Mchango kuchangia Zahanati ya Dar Pori kwa kutoa Dhahabu gramu 5 yenye thamani ya shilingi 375,000.
Mwenyekiti wa Wachimbaji Mpakani katika Kata ya Turu Nchini Msumbiji ameushukuru uongozi wa Serikali ya Tanzania kwa kudumisha Amani na Utulivu katika Mipaka ya Tanzania na Msumbiji.
Viongozi waliohudhuria Mkutano uliohusisha pande mbili za Tanzania na Msumbiji wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Viongozi wa Msumbiji wakiwa katika Mkutano wa hadhara na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na wananchi wa Tanzania waishio Mpakani mwa Msumbiji alipotembelea kujionea hali ya mahusiano katika kudumisha amani.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amesema zoezi la ununuzi wa Mahindi katika Wilaya ya Nyasa linaenda vizuri
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa wachimbaji madini kutoka Msumbiji jinsi ya kukomesha biashara ya ngono kwa watoto wadogo katika maeneo ya Machimbo.
Mwenyekiti wa wachimbaji kutoka Msumbiji amesema atahakikisha watoto wa kitanzania wanaostahili kuwa shule wanarudishwa Tanzania kwa ajili ya kuendelea na masomo .
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Inginia Dr Binilith Mahenge aiwa na mkaazi wa Dar Pori Joseph Msigwa akihoji kuhusu mapato yanayo pitishwa mpakani
Wananchi wa Dar Pori wakisikiliza Hotuba ya Mkuu wa Mkoa mhandisi Dr Mahenge wameomba kusaidiwa vifaa vya viwandani katika Ujenzi wa Zahanati wanayoijenga kwa nguvu zao.

Wazazi wakiwa katika kutano wa hadhara uliofanyika katika Mpaka wa Msumbii na Tanzania katika kata ya Unyere Tarafa ya Mpepo uliohudhuriwa na Viongozi wa Msumbiji na Tanzania ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Satano mahenge wameomba Serikali kuthibiti Mipaka na kuwakemea wafanya Biashara kuacha kuwatumikisha watoto walio chini ya miaka 18

Mmoja wa Wazazi waliotoa maoni yao wamesema wao wakiwa kama wazazi wanaona huruma kuona watoto walio chini ya miaka 18 wakifanya kazi za ngono ili waweze kujikimu na Maisha.

Mganga Mkuu wa wilaya ya Nyasa Dr Papalika akitoa ufafanuzi kwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma nama walivyowafikia wananchi waaoishi mpakai mwa msumbiji na Tanzania katika suala la huduma za NHIF
Dr Papalika amemweleza Mkuu wa mkoa wa Ruvuvuma kuhusu Ujenzi wa Zahanati unaoendelea kwa wananchi wa Machimbo ya Dar Pori kwa nguvu za wananchi.
Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kununua Tani 12 za Mahindi kutoka Wilaya ya Mbinga Vijijini, Jambo lililopongezwa kwa Serikali kuweka Vituo vya kununu Mahindi badala ya kuweka Mjini jambo ambalo lilikuwa ni adha kwa Wananchi
Viongozi mbalimbali walioambatana na mkuu wa mkoa wa Ruvuma pamoja na Viongozi utoka Nchi ya Msumbiji.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akipokea zawadi ya gramu 5 za dhahabu yenye thamani ya shilingi 375,000 ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi wa Zahanati inayojengwa na wananchi wa Dar Pori wilayani Nyasa.
Dhahabu inayopatikana katika Machimbo ya Dar Pori na Turu Nchini Msumbiji kama inavyoonekana.
Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini Nchini Msumbiji mara baada ya kukabidhi mchango wa gramu 5 za dhahabu katika ujenzi wa zahanati ya Tanzania amesea hii ni kiashiria kuwa mahusiano baina ya Nchi za Tanzania na Msumbiji ni mazuri.


Mkuu wa koa wa Ruvua Dkt Binilith Satano Mahenge amesema FRELIMO na CCM ni watu waliodumisha Amani kutokana na vyama vyao kuwa na Sera mzuri. Umoja uliojengwa kati ya Saora Mashehe na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni lazima ulindwe.

Mkuu wa Mkoa katika kudumisha Mahusiano ya undugu kati ya Wananchi wanaoishi Mpakani kati ya Msubiji na Tanzania aliweza kutembelea mipaka ya Tanzania na Msumbiji na kuweza kutambulishwa kwa viongozi walinda Mipaka ya Msumbiji.   

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dktr Mahenge akiwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Msumbiji.

Viongozi wa Msumbiji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji Msumbiji wamesema watafanya kila jinsi kuhakikisha watoto wanaoihitajika kuwa shuleni wanarudishwa Tanzania ili waweze kushiriki Masomo.
Mwenyekiti wa wachimbaji akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alipotembelea katika Machimbo ya Dar Pori yaliyopo jirani na Nchi ya Msumbiji.
Katika Ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amepata fursa ya kujionea Mpaka wa Msumbiji na Tanzania na kuomba ushirikiano ulioanzishwa na Waasisi Samora Mahehe wa Nchini Msumbiji na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uimarishwe katika kulinda mipaka yake na kudumisha mahusiano mema.
Mkuu wa Mkoa Dr Mahenge akikagua Mawe ya mpaka wa Tanzania na Msumbiji.

MKuu wa koa wa Ruvua Dkt Binilith Satano Mahenge amesema FRELIMO na CCM ni watu waliodumisha Amani kutokana na vyama vyao kuwa na Sera mzuri. Umoja uliojengwa kati ya Saora Mashehe na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni lazima ulindwe.

Mpaka wa Tanzania na Msumbiji unahitaji kuimarishwa kwa faida ya vizazi vijavyo wa maendeleo ya Nchi mbili zinazopakana. Huo ni upande wa Tanzania kama inavyoonekana.
Viongozi walioambatana na kuu wa Mkoa waipokea maelekezo juu ya Mpaka huo kutoka kwa viongozi wa Msumbiji.
Kama inavyoonyesha alama ya jiwe katika upamde wa Msumbiji mpakani mwa Tanzania.
Mipaka upande wa Msumbiji.


Viongozi wa Msumbiji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji Msumbiji wamesema watafanya kila jinsi kuhakikisha watoto wanaoihitajika kuwa shuleni wanarudishwa Tanzania ili waweze kushiriki Masomo.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Mahenge mara baada ya kukagua uimara wa mipaka katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji hapo akiwaaga wenyeji wake Askari wa Msumbiji wanaolinda usalama wa mipaka hiyo akiomgozwa na mwenyekiti wa wachimbaji.
Mkuu wa Mkoa akiagana na Askari wa Masumbiji wanaolinda Mpaka wa Tamzania na Msumbiji mara aada ya kukagua maeneo ya mipaka hiyo.
Mkuu wa Mkoa Dr Mahenge akiagana na Askari wa Msumbiji Mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji alipotembelea mpaka wa Tanzania na Msumbiji kupitia wilaya ya nyasa. Kama anavyoonekana kwa ukakamavu akiwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji kutoka Msumbiji.

Aidha katika Ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma handisi Dkt Binilith Satano Mahenge amepiga Marufuku kwa watu wanaofanya biashara ya kusafirisha watoto  ili wafanye biashara katika Mabaa na kufanyishwa Biashara ya Ngono.

Dr Mahenge amewataka Viongozi wa Vijiji, Watendaji pamoja na wananchi wa kawaida kuingia katika Vita ya kupambana na Biashara haramu ya kusafirisha watoto.


Wananchi wanaoishi mpakani mwa Msumbiji na Tanzania wameiomba Serikali kukomesha biashara ya Ngono  inayotumika kwa watoto walio chini ya miaka 17 na kusababisha watoto hao kukosa masomo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma akionyeshwa maeneo wanayo chimba madini ya Dhahabu katika eneo la Msubiji
Afisa uhamiaji kutoka Tanzania akisalimiana na Askari wa Ulinzi wa Mpaka wa Msumbiji
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Satano Mahenge akiwa katika picha ya opamoja na kaati ya Ulinzi na usalama Mkoa wa Ruvuma Tanzania na Askari Walinda Mipaka kutoka Nchini Msumbiji.

Picha ya pamoja baina ya pande mbili ikiwa ni ishara ya mashirikiano mazuri kati ya Msumbiji na Tanznia

Mwandishi wa Habari wa Star TV na Redio Free Afrika Mkoani Ruvuma Tanzania Adam Mzuza Nindi kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Msumbiji na Askari wa Tanzania katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji
Akari wa Mkoa wa Ruvuma na mwanahabari wa sblog ya songea habari wakiwa na mwenyekiti wa wachimbaji Nchini Msubij






Mkuu wa Mkoa katika kudumisha Mahusiano ya undugu kati ya Wananchi wanaoishi Mpakani kati ya Msubiji na Tanzania aliweza kutembelea mipaka ya Tanzania na Msumbiji na kuweza kutambulishwa kwa viongozi walinda Mipaka ya Msumbiji.   

WAKALA WA MISITU KANDA YA KUSINI WATOA MADAWATI 580 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 43

$
0
0

Wakala wa Misitu Kanda ya Kusini wameweza kutoa Madawati 580 katika Shule za Msingi za Mkoa wa Ruvuma, Madawati hayo yakiwa na thamani ya shilingi Milioni 43.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiwa na wanafunzi wa shule ya majiamaji akiwa uliza maswali  

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema ili kufikia uchumi wa kati, ni lazima kuimarisha miundo mbinu ya Elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha Eneo la Kusomea kuwa na Walimu wenye wito, wazazi na Serikali kushirikiana kulinda Miradi ya Elimu

Wanafunzi waliopewa Madawati  wameweza kushuuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka mikakati ya kuweza kuwafanya wanafunzi wasikae chini waweze kusoma vizuri.


Afisa Elimu Manispaa ya Songea amewaomba wazazi na Wanafunzi kulinda Madawati yaliyotokana na wadau ili Madawati hayo yaweze kudumu kwa Vizazi vingi.

Mkoa wa Ruvuma kwa kiasi kikubwa wameweza kufikia lengo la asilimia 99 ya watoto kukaa kwenye Madawati. Vita iliyopo kwa sasa ni kuhakikisha watoto wanatumia vyoo bora vyenye hali ya kisasa pamoja na kuwa na Benki ya Tofali ili kukiwa na kazi yoyote ya Ujenzi tofari hizo ziweze kutumika.

Viongozi waliohudhuria zoezi la kukabidhi adawati 580 kutoka kwa wakala wa Misitu kanda ya kusini katika Ukumbi wa Maliasili Mkoani R
mshauri wa kisheria Fatuma Misango akieleza changamoto zinazo mpata mtoto wa kike
mtalamu wa mbegu za nafaka kutoka katavi  Joanthan akitoa elimu ya jinsi ya kutumia mbegu za kisasa
Mtalamu wa mbegu kutoka katavi akitoa elimu mbegu zinazo faa koa wa ruvuma ambazo zime fanyiwa utafiti wa kutosha

Kaimu Meneja wa Wakala wa Misitu Kanda ya Kusini Embrantino Mgiye amesema pamoja na kutekeleza Amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwataka wanafunzi wote wa Shule za Msingi na Sekondari kuwa asiwepo mwanafunzi wa kukaa chini lakini Wakala wa Misitu wameona ni vyema Wananchi wafaidi Rasilimali zao kwa kutoa Madawati kwa Wanafunzi ili tupate wataalamu wazuri kwa kukaa watasoma kwa utulivu.

Kaimu Meneja wa Wakala wa misitu Kanda ya Kusini amesema utoaji wa madawati kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ni somo tosha la kuwawezesha wanafunzi  kujua kumbe misitu inasaidia kila mtu hivyo wanafunzi  wataweza kukua na kujua faida  za misitu.
mkurugenzi wa manspaa ya Songea akiwa na katiu tawala wilaya ya Songea Pendo wakati wamakabidhiano wa madawati kutoka kwa wakala wa hifadhi ya misitu kanda ya kusini

KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI AINA YA URAN YA NAMTUMBO YATOA VIFAA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 12 KWA DAWATI LA POLICE WANAWAKE RUVUMA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Dawati la Police Wanawake Anna Tembo akisoma Risala ya Mafanikio na Changamoto inalo li kabili Dawati la Jinsia Mkoa wa Ruvuma kwa Kukosa Vitendea Kazi
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge pichani akipokea vifaa vilivyoahidiwa na kampuni ya Mantra inayomilikiwa na kampuni ya Rosatom ya Urusi ambayo inahusika na uchimbaji wa madini ya uran Mkuju wilayani Namtumbo wametoa aseti za seti nne ya viti,  meza za kisasa Kompyuta,  photocopy mashine, scana, printer, TV Flat Screen,  kamera, kaunta ya vioo vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Akipokea msaada wa Vifaa kutoka kwa Afisa Mahusiano wa Mantra Khadija Pallangyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Kampuni iliyotolewa na MANTRA chini ya Kampuni ya ROSATOM ya Urusi.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge akisalimiana na Mwenyekiti wa uhamasishaji kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Ruvuma ndugu Mkude katika viwanja vya jengo Dawati la Police wanaewake Mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa kituo cha police wilaya  ya Songea akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mara alipo tembelea Dawati la Jinsia la Police Mkoa wa Ruvuma
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge  ametoa angalizo kwa jeshi la Police kuhakikisha Dawati la Police Wanawake lina kuwa  na wataalamu wanao wiana na umahiri wakuweza kutatua matatizo yanayo ikabili jamii kwa kuweka watu wenye umakini wa kufanya kazi kwa kulinda heshima na utu wa mtanzania na sio kuweka mtu yeyote ili mradi Askari pasipo kujali uwezo wake
 Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji ameahidi mbele ya mkuu wa mkoa kutoa wataalamu wenye uwezo kushugulikia dawati kwa umakini na usiri kutegemea cheocha mtu aliye kwenye dawati huku akizingatia uwezo alio kuwa nao katika kusaidia jamii.

 Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya jamii ya watanzania Renatus Martias Mkude alinukuu suala la maendeleo yaliyo tolewa na Rais Benjamini Wiliam Mkapa wa awamu ya tatu kuwa jambo jema linalo anzishwa na mtu mmoja ni budi liungwe mkono na watu wengine ili liweze kuletaufanisi na maendeleo kama hili linalofanywa na Dawati la Police katika kupinga ukatili wa kijinsia miongoni mwa jamii.
 Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia bwana Renatus Martias Mkude akiainisha mafanikio yaliyopatikana katika kuhdumia watu walio athirika na vitendo vya ukali wa kijinsia, pamoja na mama aliyekuwa anaishi Peramiho ambaye alijichongea jeneza lililovunjwa na kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia, lakini hatimaye mama huyo wiki mbili zilizopita alifariki ambapo na kamati iliweza kuchonga sanduku lingine na kumzika mama kwa ushirikiano na wananchi wa Pearamiho
 Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema utafika wakati wa kuchimba madini yaliyopo Aridhini pale tutakapowapata watanzania ambao wanaweza kusimamia na kuelekeza madini hayo ya saidie wananchi wote, Ndivyo alivyofanya dada Khadija Pallangyo kwa kusimamia kampuni ya Mantra inayomilikiwa na Kampuni ya ROSATOM ya Urusi inayochimba madini ya uran na faida inayopatikana ikilenga kusaidia jamiii inayozunguka Maeneo ya igodi. MANTRA imekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 12 chini ya Afisa Uhusiano Mzalendo Khadija Pallangyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Bilinith Satano Mahenge akisikiliza taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo iliyoainisha hali ya vitendo vya ukatili mkoani Ruvuma
 Hivyo ni vifaa vilivyotolewa na Kampuni ya MANTRA yenye makao yake makuu wilaya ya Namtumbo katka mgodi wa Urenium One Mkuju
                                                  sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa
Vifaa kama vinavyoonekana hizo ni Sacana na Printa
 Wadau mbalimbali waliohudhuria katika makabidhiano ya vifaa vilivyotolewa kwaDawati la jinsia la Police wanawake ili kurahisisha utendaji wa kazi za dawati. Kutoka kushoto ni Mussa Homera na kulia kwake ni Mratibu mhamasidhaji wa ujenzi wa jengo la dawati Bw. Juma Nyumayo
 Mdau mkubwa wa Dawati la jinsia Frenk Mchina akiwa wadau wengine akiwemo Mr Zuberi ambao wameshiriki kwa karibu katika kuchangia masuala mbalimbali ya dawati la jinsia la polisi hapo wakifuatilia utoaji wa vifaa vitakavyosaidia utendaji kwa jamii ya wana Ruvuma
 Mhamasishaji maarufu mkoani Ruvuma Meki Mguhi akiendesha mapokezi ya vifaa kutoka Kampuni ya Uranium one
 Kamati ya ulinzi na usalama wakishuhudia vifaa vikipokelewa baada ya kutolewa na MANTRA
 wadau mbalimbali wa Mkoa wa Ruvuma wanaounga mkono Dawati na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia Mkoani Ruvuma
 Kutoka kushoto ni kamanda wa Police Mkoani Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji na katikati Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge
 Picha ya Pamoja kati ya Dawati la Police Wanawake na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Binilith Satano Mahenge
 OCD na Mwenyekiti wa Dawati la kupinga ukatili wa kijinsia Anna Tembo wakipongezana kwa kuendesha Dawati la Police Wanawake
 Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili Mkoa wa Ruvuma Mkude akisalimiana na Mwenyekiti wa Uhamasishaji wa Jengo la Police Wanawake Adamu Mzuza Nindi ambaye pia ni mkurugenzi wa Blog ya Songea Habari
 Khadija Pallangyo akiwa katika Viwanja vya Police muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa kwa Dawati la Jinsia la Police Wanawake Mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando amesisitiza utoaji wa huduma kwa watu wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ameomba kamati ya ulinzi na usalama kushiriki kikamilifu katika kusimamia suala hilo
 Kamati ya Ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge
 Sehemu ya Caunter ya Dawati la Police wanawake ambayolimejengwa na kampuni ya uchimbaji wa Madini ya Uran One machimbo yaliyoko Mto Mkuju wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma

UZINDUZI SIKU NYUKI, MIZINGA 2000 YATUNDIKWA MIKOA YA KANDA YA KUSINI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Siku ya Utundikaji Nyuki Kanda ya Kusini uliofanyika katika wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma

Jumla ya Mizinga 2000 imetundikwa katika Mikoa ya Kanda ya Kusini ikiwemo Lindi, Mtwara na Ruvuma.



Kaimu Meneja wa Wakala wa huduma za  Misitu kanda ya kusini  Bowazi Sanga amesema kutokana na wananchi kujua faida ya kufuga Nyuki na wamejitokeza kwa wingi siku ya kutundika mizinga  na kufanikiwa kutundika mizinga 2000.


Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini Bowazi Sanga amewaomba Wananchi
kuitunza Misitu kwa kutochoma moto
Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu amesema kuchoma misitu moto kunasababisha
kuwakimbiza Nyuki pia kuharibu Mazingira.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Robert Magen kushoto akiwa na Afisa Ufugaji Nyuki wakitundika Mzinga katika Uzinduzi wa utundikaji wa mizinga wilayani Mbinga.
 Kulia ni Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Mkoa wa ruvuma Manyisye Mpokigwa akionyesha namna ya kutundika mizinga kwa ufasaha mbele ya wananchi wanaohitaji kunufaika na ufugaji wa kisasa.
 Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Mkoa wa Ruvuma Manyisye Mpokigwa akionyesha Mfano wa Mizinga ya kisasa kwa wale wanaotaka kuingia katika ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kujipatia kipato.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Mahenge amewaasa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujikita katika ufugaji wa Nyuki kwa kuwa hauna gharama, gharama yake ni kuchonga mizinga tu.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Mahenge amewaomba wafugaji wa Nyuki kuunda vyama vya ushirika ili wawezed kupata Soko zuri la Asali.
ufugaji wa nyuki endapo utazingatiwa unatoa tija kwa mfugaji kwa kuwa mazao yanayotokana na nyuki yananunuliwa kwa bei nzuri, ni jukumu kila mwananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiongezea kipato.
Aidha, Dr Mahenge amewaomba viongozi wa vijiji kuweka ulinzi kwenye vyanzo vya Maji kusichomwe moto, atakayebainika kuchoma moto mtu wa kwanza kuchukuliwa hatua atakuwa Mwenyekiti wa Kijiji.
Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Mhandisi Dr Mahenge akibadilishana mawazo na Maafisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini.
Wadau wa Ufugaji wa Nyuki wilaya ya Mbinga wakifurahi kusletewa uzinduzi wa Utundikaji wa Mizinga katika Kijiji cha Mahande wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akikagua mizinga kuona teknolojia iliyotumika katika kuboresha mizinga ya kisasa.
Mhandisi Dktr Binilith Mahenge katika Kijiji cha mahande wilayani Mbinga akipokea taarifa ya ufugaji Nyuki katika maadhimisho ya siku ya Utundikaji Mizinga ya Nyuki iliyofanyika kikanda wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma.

UTAFITI WA HALI YA MAAMBUKIZI YA VVU NA UKIMWI NCHINI TANZANIA KUFANYIKA KWA TEKNOLOJIA YA KISASA

$
0
0

Jumla ya watu 35,000 hufa Nchini Tanzania kutokana na Maambukizi ya VVU na UKIMWI na watoto 600,000 huachwa katika hali ya uyatima kila mwaka.


Akisoma Taarifa ya Takwimu za maambukizi ya UKIMWI  kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr. Binilith Satano Mahenge  amesema Takwimu ni kubwa hivyo ili kuweza kupunguza ongezeko  hilo  inabidi kutumia njia shirikishi itakayo kuwa na idadi sahihi ya maambukizi 

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Mihayo Bupumba amesema njia ya kwanza ni kuhakikisha wale wote walioathirika wanajulikana kwa asilimia 90%, njia ya pili ni kutambua kama hao walioathirika wanapata dawa za ARV kwa asilimia 90%  njia nyingine ni kufahamu na kudhibiti maambukizi mapya kwa asilimia 90% kwa kufanya sense ya kitalamu bila kumlazimisha mtu

 Katika utafiti huo Mkoa wa Ruvuma utahusisha katika wilaya zote kinachotakiwa ni wale wanaotakiwa kuwakilisha kushiriki kikamilifu.
 Wadau wa Mapambano dhidi ya ukimwi kutoka halmashauri za Mkoa wa Ruvuma, Taasisi za Dini na Asasi zinazoshughulika na masuala ya UKIMWI wakiwa katika mkutano wa kupokea taarifa ya Utafiti wa Viashiria vya Ukimwi unaotarajia Kufanyika Tanzania nzima kwa kaya wakilishi.
 Wadau wamesisitizwa kutoa ushirikiano katika zoezi hilo muhimu ili kufahamu Takwimu sahihi za hali ya maambukizi zitakazosaidia Serikali kujua namna ya kupanga Bajeti katika kuhudumia waathirika wa VVU
 Wataalamu wa Afya kutoka Kitengo cha Utafiti wa Viashiria vya VVU na UKIMWI
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akitoa taarifa ya namna walivyoandaa maeneo yatakayohusika na utafiti huo kwa kushirikiana na waratibu na watakwimu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Mihayo M. Bupamba akielezea teknolojia itakayotumika katika utafiti kwa kutumia electronic ambayo itatoa usahihi wa data.

ZIARA YA KAMISHINA JENERALI WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOANI RUVUMA

$
0
0


Kamishina  Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Tanzania Thobias Andengenye amewataka amewataka Askari wa Zimamoto kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa uaminifu ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya Tano.



Kamishna  Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma, amesema Ziara yake inalenga kutaka kujionea changamoto zinazolikabili Jeshi la Zimamoto.



Akizungumzia kuhusu Vifaa vya kuzimia moto na jinsi ya kutoa Elimu kwa wananchi ili wasiweze kupatwa na Majanga ya moto amesema, ni vizuri unapopata kiwanja kabla ya kujenga ukawasiliana na Viongozi wa Zimamoto na uokoaji ili wakupe elimu jinsi ya kuepukana na Majanga yanayotokana na Moto.

Askari wa Zimamoto Briged ya kusini 401 KV wakitoa heshima kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na ukoaji akiwa Ziarani Mkoani Ruvuma.


Kamishna Jenerali  wa Zimamoto Thobias Andengenye akielezea kuhusu Vifaa vya kuzimia moto katika maghari, ametoa ufafanuzi kuwa fedha zinazolipwa TRA ni kwa ajili ya ukaguzi na sio za kununulia mitungi ya gesi. Jambo linalowachanganya wengi.



Kamishna  Jenerali wa Jeshi la Ziamamoto na Uokoaji amesema kwa hivi sasa changamoto inayolikabili Jeshi la Ziamamoto ni kukua kwa miji ambako ujenzi hauzingatii kujikinga na majanga.

Amesema kiutaratibu kinachotakiwa kila baada ya kilomita 15 kuwe na kikosi cha zimamoto.
Askari wa Jeshi la Ziamamoto na Ukoaji wa kikosi cha Briged ya kusini 401 KV wakiwa katika Ofisi za Kikosi hicho Manzese Manispaa ya Songea.
Vitendea kazi vya Jeshi la Zimamoto uokoaji vinavyotumika pindi majanga ya moto yanapotokea.
Magari ya Zimamoto yakiwa katika eneo la Kikosi cha Jeshi la Ziamamoto na uokoaji manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Askari wa Jeshi la Zimamoto wametakiwa kushirikiana na Vyombo vya habari katika kutoa Elimu ya kujikinga na Majanga ya moto badala ya kusubiri majanga yatokee kwa kuwa wao ndio wana wajibu wa kuzuia majanga kwa kuelimisha jamii kujikinga na majanga ya moto.

MIZINGA UTUNDIKAJI STORY TWO

contenental


UPANDAJI WA MITI MADABA

MAMBO MHIMU KATIKA MAISHA KUZALIWA,KUBATIZWA,KUPATA KIPAIMARA NA KUOA,MWISHO KIFO

$
0
0
Bwana Harusi na Bibi Harusi wakiwa katika mlango wa kanisa la mji mwema manspaa ya songea
Bi Harusi Cristina Ngonyani akiwa tayari kutia sahihi cheti cha ndoa kuonyesha kuridhia kuolewa na na Staniley Matembo
Bwana Harusi Staniley Matembo akitia sahihi katika cheti cha Ndoa kuridhia kumwoa Cristina Ngonyani
Hapo bwana  Harusi Staniley Matembo akitia sahihi mbele ya padri kukubali kumwoa Cristina Ngonyani
                          Padiri wa Mji Mwema akitoa vyeti kwa bwana harusi na bi Harusi
vyeti hivyo bwana hapo ndoa tayari hebu angalia bi harusi na bwana harusi wanavyo furahia ndoa
Bi harusi Cristina Ngonyani kulia akiwa amekaa na bwana wake Satiniley Matembo wakiwa kanisa la mji mwema
Siku aliyo funga ndoa Staniley Matembo kulikuwa na ndoa zisizo pungua tatu
vinubi vinanda na nyimbo ni moja ya kumushkuru Mungu kwa kufanikisha ndoa za watu wa
                                        Hao hi kufunga ndoa katika kanisa la mji mwemani maharusi walio wa

maharusi wakipiga picha ya pamoja na padri wa mji mwema mara baada ya kutoa baraka
MOJA YA FURAHA YA MAHARUSI NI KUONA TABASAMU YA WATU WALIO WASINDIKIZA
 Harusi ni njia moja ya kukubaliana kuwa uta ishi na mwenzio bila kinyongo na wote kuwa mwili mmoja huku watu wakishudia kama unavyo waona hawa hapa
 Hapo ni nyumbani mji mwema wakiingia kwenye nyumba yao chini kukiwa kumetandikwa kanga ishara ya upendo
 Hiyo ni harakati ya kuingia nyumbani Mjimwema Mapacha wakiongoza msafara wa Harusi
 Harusi ni mafunzo kwa watoto hapo Staniley Matembo akiwa na Bi Harusi Cristina Matembo akiwa na Mapacha wao wakisindikiza Harusi
Mara baada ya kutoka kanisani bwana harusi Staniley Matembo alipokelewa kwa furaha nyumbani kwake Mjimwema akiwa na bi harusi Ceistina Ngonyani

utalii katika ziwa nyasa story

NAIBU WAZIRI WA ELIMU,SAYANSI,TEKNOLOJIA, NA MAFUNZO YA UFUNDI MHANDISI STELA MANYANYA AWAHIMIZA WATANZANIA KUJA KUONA VIVUTIO VITATU MARUFU VILIVYO TUMIKA WAKATI WA VITA VIKUU VYA PILI VYA DUNIA KWA WATU KUJIFICHA KATIKA VISIWA HIVYO NA KINGINE KUTUMIKA KUHIFADHI WAGONJWA WA UKOMA WAKATI WA MKOLONI

$
0
0
Ziwa Nyasa ni moja ya Maziwa Ulimwenguni ambalo lina Maji Baridi na Matamu ukiachana na utamu wa Maji bado una toa Samaki wa tamu ambao wamekuwa na sifa katika jamii. Samaki hao ni Mbasa,Mbelele,Mbufu, Nin'gwi,pamoja na Magege,Vituhi,na Dagaa nyasa ukifika ziwa nyasa uliza hao Samaki utapata uhondo.
Katibu wa Naibu waziri wa Elimu sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Yonafika Mzungu akishuhudia uzuri wa Ziwa Nyasa na maajabu yake ikiwemo na vivutio vyenye mandhari nzuri alipokuwa ziara katika Ziwa Nyasa na Naibu waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya.


Naibu waziri wa elimu,sayansi,Teknolojia, na Mafunzo ya ufundi Mhandisi Stella Manyanya  amewaomba watanzania kushiriki katika maadhimisho ya utalii yatakayo fanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu. Pichani ni watalii wa ndani wakiongozwa na Naibu waziri wa Elimu wakiwa katika Boti kutembelea visiwa mbalimba vinavyopatikana katika Ziwa Nyasa.

Mhandisi Stella Manyanya amesema ukitembelea mwambao wa ziwa Nyasa utaweza kufaidi vivutio vilivyoko katika ziwa nyasa na kupata vyakula vya asili ikiwemo samaki wanaopatikana katika Ziwa hilo wenye ladha safi ya asili.
Miongoi mwa vivutio vilivyopo katika visiwa vya ziwa nyasa ni pamoja na mawe mazuri na maeneo ambayo wavuvi hupata hifadhi pindi ziwa linapochafuka. Hicho ni kisiwa cha Lundo kilichopo Mbamba Baye kilomita chahe kutoka Nchi kavu.

Katibu Yonafika Mzungu kutoka Ofisi ya Naibu waziri wa Elimu akichukua kumbukumbu ya mambo yanayopatikana katika kisiwa cha Lundo Mbambabay wilayani Nyasa.
Pamoja na mazuri mengi yanayopatikana Ziwa Nyasa pia kuna dagaa wenye stata ya aina yake almaarufu Dagaa Nyasa kama wanavyoonekana pichani wakiwa wameandaliwa katika mitungo tayari kwa kukaushwa ili waliwe ukiwapata wakiwa wametengenezwa utapenda uwatumie mara kwa mara. kulia ni Naibu waziri Mhandisi Manyanya akishuhudia utajiri wa Mwambao wa Ziwa Nyasa.

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia, na Mafunzo ya ufundi Mhandisi Stella Manyanya  amesema kuvijua vivutio vya mwambao wa ziwa nyasa ni fursa kwa wananchi kuzitambua rasilimali ambazo zinaweza kuwaingizia kipato.
Mhandisi Manyanya amesema utalii wa ndani una faida na fahari  kwa kuwea utaweza kujifunza mambo mbali mbali ya Historia ya Ziwa Nyasa ambayo yakitangazwa ipasavyo ni faida kwa wakazi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa, Mkoa na taifa kwa ujumla. Piachani ni Msafara wa Naibu Waziri wa Elimu wakielekea katika kisiwa cha Lundo kwa usafiri wa Boti.
Ziara ya Naibu waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya katika kutembelea vivutio vilivyopo katika Ziwa nyasa ilipiga kambi katika Kisiwa cha Lundo kupata historia ya kisiwa hicho ambacho kilitumika kama makazi ya wagonjwa wa ukoma baada ya kutengwa na familia zao kutokana na ugonjwa.

Naibu waziri wa elimu,sayansi,Teknolojia, na Mafunzo ya ufundi Mhandisi Stella Manyanya  akielezea kuhusu kisiwa cha lundo kilichopo wilaya ya nyasa amesema kisiwa hicho kinaitwa kisiwa cha lundo Mkombozi kutokana na kuwa kimbilio kwa wavuvi wanapopatwa na dhoruba wakiwa katika shughuli za uvuvi Ziwa linapochafuka hujificha kisiwani hapo na kusalimika.

Hayo ni mawe ya aina yake yenye kuvutia ambayo unayapata katika Kisiwa cha Lundo katika ziwa Nyasa ambapo utaweza kupafikia kwa kutembea kwenye maji umbali usiopungua mwendo wa nusu saa kwa usafiri wa Boti au Mtumbwi kutoka Nchikavu . Ni mawe yenye nakshi ya rangi nyeupe pembeni utadhani yamepakwa rangi.


Naibu waziri wa elimu,Sayansi,Teknolojia, na Mafunzo ya ufundi Mhandisi Stella Manyanya  akiwa katika ziwa nyasa kujionea vivutio vilivyopo kwenye ziwa hilo ikiwepo ufukwe, kisiwa cha lundo ambacho wakati wa ukoloni kilitumika kama kambi ya wagonjwa ukoma.

Kutoka kushoto mwenye life jaket ni Meneja wa TANSCO Kanda ya Kusini Joyce Ngahyoma, katikati Mhandisi Stella Manyanya na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba wakifurahia mandhari nzuri ya Mwambao wa Ziwa Nyasa na hali safi ya hewa walipotembelea kisiwa cha Lundo katika Ziara ya Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na taknolojia Mh Manyanya.
Hivyo ndivyo wakaazi wanaozunguka ziwa Nyasa wanavyoona fahari kutumia Rasilimali Hadhimu ya Ziwa Nyasa wakiwa katika mtumbwi kuelekea kutafuta ridhiki katika ziwa lao hakika ni fahari kuwa na tunu ya aina hiyo.
Mwonekano wa Ziwa Nyasa na Maji ya kupendeza pembeni kukiwa na uoto wa asili.
Uzuri wa Ziwa Nyasa unaambatana na Visiwa vyenye mvuta na historia ya aina yake hicho kinachoonekana kwa mbali ni kisiwa cha Lundo ambacho kina historia ya aina yake kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Unapofika Ziwa Nyasa huna hofu ya kukuwezesha kufika katika kisiwa chochote kujionea uzuri wa Ziwa hilo na yanayopatikana katika fukwe na visiwa vinavyovutia kuvitembelea kuna usafiri wa boti kama unavyoiona pichani na manahodha wenye ujuzi wa kuziendesha pia kuna mitumbwi kwa ajili ya kusafirisha watu.kwenda upande wowote wa ziwa hilo.
Boti la kisasa linalotumika kusafirisha Abiria wa Majini katika pande zote za ziwa Nyasa kama unavyoona wataalamu wakiliendesha kuelekea maeneo ya visiwa vilivyopo Ziwani.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Kusini Joyce Ngahyoma akiwa katika ziwa Nyasa kujionea usuri wa Ziwa hilo maarufu Duniani lenye utajiri wa vivutio ambavyo maeneo mengine havipatikani.
Maji ya Ziwa Nyasa ni Maangavu yenye kuvutia ambayo ukiangaza unaweza kuona vitu vilivyo chini kama inavyoonekana katika picha.
Ukifika Ziwa Nyasa utakutana na nakshi ya mawe tofauti tofauti yenye kuvutia kama inavyoonekana pichani hapo ji kandokando ya kisiwa cha Lundo hakika ni nadhifu.
Naibu Waziri wa Elimu Mbunge wa Jimbo la Nyasa akifafanua juu ya umuhimu wa kuhifadhi na kuvilinda vivutio vya Ziwa Nyasa ikiwemo Fukwe na Visiwa kwa kutouza badala yake viwekwe safi kwa ajili ya utalii kwa wageni wa ndani na nje ya Nchi jambo ambalo litasaidia kuongeza pato kwa wakazi wa mwambao na Taifa.
Watalii wa ndani waliokuwa katika Ziara na Naibu Waziri wa elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Manyanya wakiwa katika piacha ya pamoja kando kando mwa Ziwa Nyasa katika Kisiwa cha Lundo Mbamba Bay wilayani Nyasa.
Nahodha Emmanuel Mguhi akihakikisha usafiri wa boti kama uko sawa tayari kwa kusafirisha Abiria wanaotoka Nchi kavu kwenda ziwani na katika visiwa vilivyopo katika Ziwa Nyasa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Nyasa hakuwa nyuma katika Ziara ya Naibu waziri wa Elimu kuhakikisha Usalama unakuwepo hata katika Maji aliongoza msafara wa Naibu waziri katika Visiwa na fukwe mbalimbali alizotembelea.


Mkuu wa vilaya ya Nyasa amesema kisiwa cha lundo kina vitu vingi vya kujivunia yakiwemo mapambo ya maganda ya konokono ambayo yanaweza kutumika kama mkufu, pia kuna samaki wa mapambo na mawe ya kuweza kupumzika. Mkuu wa wilaya amesema wilaya ya Nyasa ina wasomi wengi wanaotoka mwambao wa ziwa Nyasa ni juu yao kushirikiana kwapamoja  kuenzi na kutangaza kuhusu utalii wa ziwa Nyasa

Mhandisi Stella Manyanya amewaomba watanzania na wazawa wa Ziwa Nyasa kuja kushuhudia visiwa vilivyoko katika ziwa nyasa ikiwemo pomonda visiwa vilivyo tumika kwa watu kujificha wakati wa vita vya pili vya dunia, pia kuona mawe mawili  Jike na Dume yanayo tumika kutambikia wakati wa shida. Hayo Maji ya kuvutia yenye rangi nzuri kama yanavyoonekana pia yanapatikana Ziwa Nyasa .
Mawe yanayopatikana katika ziwa Nyasa yakiwa na naksh asili ya rangi ya kijani.

Naibu waziri wa elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya ufundi Mhandisi Stella Manyanya  amewaomba wazawa na watanzania wote kushiriki katika sherehe zitakazofanyika Desember 30 mwaka huu.  wa shida

Yonafika mzungu Katibu wa Naibu waziri wa Elimu Mahandisi Manyanya akifaidi uzuri wa fukwe za Ziwa Nyasa alipokuwa Ziara ya kikazi Wilayani Nyasa.
Mkuu wa Kituo cha Maliasili Utalii na Ufugaji Geofrey Sakala akiwa na Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya wakitafakari jinsi ya kuboresha vivutio vilivyopo katika mwambao wa Ziwa Nyasa ambavyo ni vya asili na utamaduni.

CHAMA CHA AKIBA SACOS YA WALIMU MANISPAA YA SONGEA YAPATA FAIDA YA SH MILION 14 KTK KIPINDI CHA JAN HAD OKTOBER 2016

$
0
0


Wanachama wa Sacoss ya Walimu Manispaa ya Songea yenye Wanachama 320 imeweza kuwakopesha wanachama kiasi cha Shilingi Bilioni 3,931,780,000/


Mwenyekiti wa Sacoss ya Walimu Manispaa ya Songea Antony Mahundi amesema Saccos ya Walimu imeweza kupata faida kutokana na Wanachama wake kukopa na kurudisha mikopo kwa wakati. Jumla ya Shilingi Milioni 14 na laki 6 imepatikana na kuweza kuendesha Mkutano Mkuu bila kukopa mahali


Mgeni rasmi Godrey Majuto akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea katika mkutano huo wa chama cha kuweka na kukopa cha manispaa ya songea amewataka viongozi kutoa elimu kwa wanachama wapya ili kuongeza Idadi ya wanachama na huduma za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujikwamua katika masuala mbalimbali ya maendeleo.



Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo Sacos ya Walimu wa Manispaa ya Songea Antony Mahundi amesema katik kutafuta washindi waliongoza kurejesha mikopo kwa wakati jumla ya wanachama 7 waliweza kurejesha mikopo kwa wakati ambao walishindanishwa na kupatikana washindi watatu walifanya vizuri zaidi.



Katibu wa Chama cha kuweka na kukopa cha walimu wa Manispaa ya Songea Gebhard Nyoni akielezea hali ya mapato na matumizi yaliyopatikana katika chama hicho kwa mwaka 2016  amesema katika kipindi  cha January hadi Oktoba Chama kimeweza kukusanya kiasi cha Tsh. 60,886,811.38 na kutumia kiasi cha shilingi 46,642,959.10



Amesema Makusanyo hayo yamepatikana kutokana na faida ya mikopo shilingi 46,684,692.64, viingilio vya Wanachama 100,000.00,makusanyo toka uwekezaji Tsh, 13,816,800.00 na Mapato mengine ikiwa ni Tsh 285,318.00.



Wanachama waliokopeshwa na kuweza kurudisha kwa wakati ambao walioshindanishwa na kushinda 3 wamesema mikopo imeweza kuwasaidia kusomesha watoto hadi chuo kikuu . Sacoss ya Walimu wa Manispaa ya Songea pia imeweza kutoa rambirambi kwa wafiwa kiasi cha shilingi Milioni 6,300,000 kati ya shilingi  24,678,328.50 zilizotengwa.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AKIWA ZIARA WILAYANI NYASA MKOA WA RUVUMA

$
0
0


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medard Kalemani amesema nyumba nyingi zinazoungua kwa ajili ya Umeme ni makosa yanayotumika kwa kutumia  Mafundi Vishoka, kutandaza nyaya za umeme pasipo na ujuzi.

Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Kusini Joyce Ngahyoma akiwa katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Ruvuma


Naibu Waziri amewaomba Wananchi kuacha kutumia Mafundi umeme wasio na sifa, wakandarasi wote wanaohusika na ufungaji  umeme majina yao yabandikwe katika mbao za matangazo ili mwananchi aweze kujua fundi kamili ni nani.



Naibu Waziri wa Nishati na Madini akiwa ziara wilayani Nyasa amewaambia wananchi wa wilaya ya Nysa kuwa  REA awamu ya tatu inaanza kwa kasi ambapo vijiji vyote ambavyo havina umeme vinatakiwa kufungiwa umeme ikiwemo na vijiji vya wilaya ya Nyasa.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medard Kalemani  amesema ili kuharakisha zoezi la kufunga umeme linafanyika kwa wakati Viongozi wa TANESCO wanatakiwa kuweka vituo katika Kata  na vijiji ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kurahisisha kupokea malipo kwa wateja wanaounganishwa badala ya  wananchi kufuata huduma Mbamba Bay.



Wananchi wa mwambao wa ziwa nyasa wameishukuru Serikali kuleta umeme wa Rea wamesema itasaidia kupata mwanga vijijini pia katika biashara ya samaki na dagaa wanavuliwa Ziwa Nyasa wataweza kuhifadhi  katka majokofu na kusafirisha salama pindi wanapokwenda kuuza nje ya wilaya pamoja na  kukuza uchumi kwa kufanya shughuli zinazohitaji umeme.

Meneja wa TANESCO wilaya ya Nyasa akifuatilia kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini katika kutekeleza Mradi wa REA awamu ya tatu wilayani humo.


Afisa tawala wa wilaya ya nyasa Richard Mbambe akimweleza naibu waziri wa Nishati na Mdini amesema kati ya vijiji 94 vya wilaya ya nyasa ni vijiji 7 tu ndivyo vilivyo na umeme wa Rea hivyo juhudi zina takiwa kuvifikia vijiji vilivyo baki


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr. Medard Kaleman amesema katika Mkoa wa Ruvuma watu ambao hawajafungiwa Umeme wa REA  wanafikia zaidi ya 3000 na ifikapo 2018 kila Kijiji kitakuwa umeme. Naibu waziri wa Nishati ametoa angalizo kwa kiongozi yeyote wa Shirika la TANESCO atakayeshindwa kumfuata Mwananchi basi atakuwa amejiondoa mwenyewe kazini

MKUU WA WILAYA YA SONGEA POLOLET MGEMA AMEPIGA MARUFUKU WANANCHI KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KATIKA HIFADHI YA MILIMA YA MATOGORO

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Songe amepiga marufuku kwa Wananchi kufanya shughuli za kibinadamu katika Eneo lililopimwa kwa ajili ya Hifadhi ya Milima ya Matogoro lenye Ukubwa wa Hekta 6755.


Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema  ameyasema hayo baada ya Wananchi wa Kijiji cha Kikunja kukataa kuweka Mipaka ya hifadhi ya Misitu kwa madai kuwa Hifadhi ikipimwa Wananchi wananyanyaswa na Maliasili kwa kupigwa na kukatazwa kusogea katika Mipaka hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akikagua Hifadhi ya Milima ya Matogoro Kusini ametoa Agizo kwa Mtu yeyote atakayeonekana akifanya Shughuli za kibinadamu katika Hifadhi hiyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani
 kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Songea ikiongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Songea Mgema wakiw katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wa kijiji cha kikunja na uongozi wa kata ya Matimila  pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu katika Kijiji cha Kikunja Songea Vijijini
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kikunja katikati Teodat Ansgar Kwanji akipokea Agizo toka kwa Mkuu wa Wilaya juu ya kusimamia ulinzi wa vyanzo vya maji katika hifadhi ya misitu kwenye eneo lake ambalo wananchi walizuia wakala wa misitu kuweka mipaka ya hifadhi hiyo kisheria
 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kikunja Teodat Ansgar Kwanji amemuomba Mkuu wa wilaya

kuitisha mkutano wa hadhara kwa Wananchi ili kutoa Elimu juu ya Mipaka kwa kuwa Wananchi hawana Mihutasari inayoainisha uwepo wa Mipaka.
  Eneo la Hifadhi katika safu ya Milima ya Matogoro Magharibi
 Sehemu ya eneo la Msitu wa Matogoro ambalo ni chanzo kikubwa cha maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea
 Wananchi wa Kijiji cha Chikunja Kata ya Matimila Tarafa ya Muhukulu
 Wananchi wa Kata ya Kilagano waliokuwa wanafanya shughuli za Kilimo katika eneo la Hifadhi ya misitu
 Sehemu ya eneo la hifadhi Kata ya Kilagano lililoingiliwa na wakulima kufanya shughuli za Kilimo
 Afisa Mtendaji kata ya Matimila Emmanuel Njogopa akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Wilaya jitihada walizozichukua katika kusimamia eneo la hifadhi ya misitu.
 Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Songea Manyisye Mpokigwa akiratibu sheria za uhifadhi na nini wananchi wanruhusiwa kukifanya eneo la Hifadhi amesema ni kosa kufanya shughuli za kilimo na kukata miti mibichi.
 Wananchi wa Vijiji vya Kihagala, Muungano Zomba na Kilagano wamesema eneo wanalolima walirithi kwa mababu toka zamani wameomba Serikali kuwafikiria kwa kuwa hawana maeneo mengine ya kulima wamesema wapo tayari kushirikiana na Serikali kwa kupanda miti na kuilinda.
 Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema katikati akibadilishana mawazo na viongozi wengine juu ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na wananchi kuingilia hifadhi ambazo ni vyanzo vya maji yanayotumiwa na wakaazi wa Wolaya ya Songea. Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Songea Pendo Daniel
 Viongozi wa Kata ya Kilagano wakiratibu maelekezo toka kwa Mkuu wa wilaya ya Songea namna wanavyopaswa kusimamia sheria katika kuhifadhi misitu na vyanzo vya maji kwenye maeneo yao.

Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Songea Manyisye Mpokigwa  ameainisha shuguli zinazopaswa kufanyika katika eneo la hifadhi ambazo haziathiri vyanzo vya maji na uharibifu wa Mazingira.


Eneo la Hifadhi ambalo halijapimwa lenye ukubwa wa Hekta 3208 ni miongoni mwa maeneo ya Vyanzo vya Maji ambavyo ni tegemeo kwa wakazi wa Manispaa ya Songea.

MBUNGE WA JIMBO LA NYASA MHANDISI STELLA MANYANYA ANAWAKARIBISHA WADAU WOTE KATIKA TAMASHA LA UTALII KUFANYIKA DESEMBER 30 WILAYANI NYASA

VYOMBO VYA HABARI VYA SAIDIA KUWAKOMBOA WANANCHI KATIKA KUWADHULUMU WAJANE NA WAGANE KATIKA KUPATA HAKI ZAO

$
0
0


Mkuu wa Wilaya ya Makete Mkoani Njombe Veronica Kessi  amewaomba Wananchi ili kuepukana na dhuluma inayofanywa na Jamii kwa kupora Mali za wajane na wagane suluhu yake ni kushirikiana vitendo vinavyotoa Msaada wa Kisheria kwa Wananachi ambao hawana Elimu hiyo, Pamoja na kutoa habari zao za kudhulumiwa kwenye vyombo vya habari.

Mkuu wa Wilaya ya Makete ameyasema hayo baada ya Wagane na Wajane 80 kupata msaada wa kisheria na kuweza kurudishiwa mali walizoporwa.
Mkuu wa Wilaya ya Makete Veronica Kessi amesema wilaya ya Makete ina Kata 23 na katika Kata hizo kata 22 zina wasaidizi wa kisheria ambao wamekuwa msaada kwa wasiojua sheria wakishirikiana na vyombo vya habari  za kitaifa pamoja na vyombo vya wilaya ikiwemo  Green FM na Kituro FM

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amesema anashukuru vyombo vya habari kwa kuwa wameweza kusaidiana na wananchi katika kupunguza migogoro mbalimbali inayowakabili wananchi kwa kutangaza  hatua zinazochukuliwa na Serikali baada ya kuona wajane na Wagane wakitaka kudhulumiwa mali zao.
Mkuu wa wilaya ya Makete amesema kuwa na wasaidizi wa kisheria kwa Kata 22 za wilaya ya Makete kumeleta mwanga kwa wasiojua sheria  kusaidiwa na kupata haki zao ikiwemo kurudishiwa mali zao.

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amelipongeza Shirika lisilokuwa la kiserikali la PADI  likishirikiana na shirika la Msaada wa Kisheria SOPSE  kutoa Elimu kwa wasaidizi wa kisheria  na kuweza kufuzu vizuri katika utetezi huo, amesema wilaya itaendelea kusaidia Asasi zinazounga mkono shughuli za Maendeleo ikiwemo PADI

Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema wafadhili baada ya kuona PADI ilivyofanya vizuri katika mwaka mmoja uliopita wameongezewa ufadhili kwa miaka mi nne na kuongeza wigo wa utoaji huduma kutoka wilaya moja ya Makete hadi kufikia wilaya tano za Mkoa wa Njombe.

Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema vitendo vya kudhulumu wajane na wagane katika wilaya ya Makete vilikuwa vingi mno kiasi cha kuwaacha watoto waliofiwa na wazazi wote wawili kuishi kwa matatizo jambo lililosababisha ongezeko la watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi.
Shirika la PADI limeweza kufikisha Elimu kupitia vitengo vya kisheria na kuweza kusaidia watu 80 waliopatwa na majanga ya Mirathi, ndoa na masuala ya kumiliki Ardhi.

Mkurugenzi wa PADI ameomba pamoja na washauri wa kisheria wameweza kufanikiwa katika kazi hiyo lakini msaada wa vyombo vya habari kama inavyofanya Radio Free Africa , Green FM na Kitulo Fkujitolea kutangaza matukio yanayowapata Wagane na wajane kwa kutangaza bure, na vyombo vingine viige tabia hiyo.


Mkurugenzi  Mtendaji Halimashauri ya Makete Gregory Emanuel amesema katika kupata kituo hicho sasa suala la Maendeleo liko mbele kwani migogoro ya Ardhi sasa imepungua , kwa kiasi kikubwa sasa  wananchi wanashiriki kazi za Maendeleo. Migogoro inashughulikiwa na wasaidizi wa kisheria kwa njia ya upatanishi.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Makete Felex Mbwiro  amesema kazi ya Afisa Maendeleo ni kuhakikisha hakuna Mwananchi anayekosa Maendeleo kwa ajili ya kunyanyaswa kwa kudhulumiwa mali zake, akiungwa mkono na Afisa Idara ya maji jinsi vitengo vya kisheria vinavyosaidia wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amewaomba wananchi na Viongozi wa Serikali kutofumbia macho vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa wananchi kwa kudhulumiwa mali zao na familia za wajane na wagane baada ya mme au mke wa marehemu kufariki. Na kuwataka waache kudhulumu mali za familia ya marehemu aliyefariki badala yake wawe wasimamizi kuhakikisha hakuna anayeingia na kudhulumu mali hizo.


MKUU WAWILAYA MAKETE NA MSAADA WA KISHERIA STPRY

MKUU WAWILAYA MAKETE NA MSAADA WA KISHERIA STPRY

MKUU WA MKOA NA MICHEZO NYASA STORY

Viewing all 441 articles
Browse latest View live